Matangazo



MATANGAZO MUHIMU
1. Kwa wale mlioahidi michango kwa ajili ya madhabau ya BWANA. Mnakumbushwa kufikisha michango yenu.

Kuhusu USCFMUST


U.S.C.F. Ni umoja wa Kikristo wa wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania unaolelewa na makanisa yaliyo chini ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania yenye makao makuu Dodoma nchini Tanzania. Tawi la USCF-MUST lilianza rasmi nwaka 2009 likiwa chini ya mwenyeki ABEL WILSON MAKALA. Kabla ya kujiunga na jumuiya hii ya vyuo vikuu chuo kimepitia katika hatua ikiwa chini ya Umoja wa Kikristo wa Wanafunzi Tanzania (UKWATA) wakati huo chuo kikiwa kinaitwa Chuo Cha Ufundi Mbeya (MBEYA TECHNICAL COLLEGE-MTC) na baadaye kikiwa Taasisi Ya Sayansi na Teknolojia Mbeya(MBEYA INSTITUTE OF SCIENCE AND TECHNOLOGY-MIST). Kama chuo kikuu sasa na hata kabla ya chuo kikuu uongozi wa UKWATA wa wakati huo ukaona ni vyema kujiunga na UMOJA WA WANAFUNZI WA KIKRISTO WA VYUO VIKUU TANZANIA kutokana na kuwa na ratiba ya tofauti ya chuo ambayo haiwapi mwanga wanajumuiya hii kushiriki kikamilifu sana katika ratiba za UKWATA. Hii ilisababisha wanafunzi wengi wa UKWATA wa kipindi kile kutokupata chakula hasa cha kiroho kutoka kwenye makongamano mbalimbali ya kitaifa na kimkoa, kwa hiyo uongozi wote kwa kushirikiana na vyuo vya mkoa wa Mbeya wakaona ni vyema kutafakari kwa makini ni namna gani tuingie kwenye Jumuiya itakayotupa nafasi ya sisi pia kuwa washirika wa karibu na vyuo vingine kutuleta pamoja kama wanavyuo wa Kikristo. Lakini pia changamoto ya rika na matakwa ya wanachuo baada chuo na wanafunzi baada ya sekondari ilikuwa ni moja ya sababu ya kufanya tuangalie namna ambavyo tutawafanya wanachuo wengi kupata mafundisho yanayoendana na umri na matakwa yao ukilinganisha na wanafunzi wa sekondari. Kutokana na sababu hizi viongozi wa UKWATA wakati huo ukaona ni vyema kujiunga na Jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vikuu Tanzania.

Baada ya kukubaliwa kujiunga na umoja huu wa vyuo vikuu, tumepita katika vipindi vya kiuongozi. WAFUATAO NI VIONGOZI WA USCF MUST KUTOKA ILIPOANZISHWA.

  1. 2009-2010- ABEL MAKALLA
  2. 2010-2011-DANIEL ISAYA
  3. 2011-2014-PENIEL SARAKIKYA
  4. 2014-2015-GOODLUCK A. MUSHI
  5. 2015-2016-TUMSIME NGABONA
  6. 2016-2017-MWAIKENDA MICHAEL

USCF tawi la MUST inajihusisha na masuala yote ya kiroho na kijamii ndani na nje ya chuo. Malengo mapana ya USCF-MUST Ni kuhakikisha inawabadili wanafunzi na kufuata njia za YESU kristo kama bwana na mwikozi wa maisha yao. Lakini nje ya kutangaza injili pia inapenda kuwa sehemu ya suruhisho la masuala yote ya kijamii na kiuchumi yanayoizunguka jamii husika. TUNAPENDA KUWA WATATUZI WA MATATIZO SIO WATENGENEZA MATATIZO.

MUNGU IBARIKI USCF.

MUNGU IBARIKI TANZANIA

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni